Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma leo amekwenda mahakama kupinga jaribio jipya la kutaka kurejeshwa kwa mashtaka 783 ya rushwa yanayohusiana na mikataba ya silaha ya 1990.

Chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance (DA), kimekwenda mahakamani mara 11 tangu mwaka 2009 ili kushinikiza kufunguliwa mashitaka juu ya mikataba ya kijeshi iliyofikiwa baada kumalizika utawala wa ubaguzi wa rangi na utengano nchini Afrika Kusini ambayo yamemzonga Zuma kwa sehemu kubwa ya muda wake wa uongozi.

Mwaka 2005 aliyekuwa mshauri wa masuala ya fedha wa  rais Jacob Zuma, Shabir Shaik alitiwa hatiani kwa kuwezesha utoaji wa hongo kwa kupatiwa mikataba hiyo na alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani.

Baadaye aliachiliwa kutokana na sababu za kiafya. Rais Zuma na maafisa wengine wa serikali yake walituhumiwa kupokea rushwa kutokana na manunuzi ya ndege za kivita zenye thamani ya dola bilioni 5 pamoja na boti za doria na silaha nyingine kutoka kwenye makampuni matano ya barani Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *