Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amemfukuza Waziri wa fedha Pravin Gordhan pamoja na naibu wake Jonas Mkabisi ambao ndio waliokua sababu kuu ya kuwepo mabadiliko ya sasa.

Taarifa kutoka ikulu ya Afrika Kusini zinasema Malusi Gigaba ameteuliwa kuwa waziri mpya wa fedha.

Takriban mawaziri 15 wametimuliwa katika kile kinachotajwa kama mshangao kwa serikali ya Zuma.

Mapema wiki hii Gordhan aliamriwa kurudi nyumbani kutoka London alipokwenda kwa ziara ya kikazi, baada ya kutuhumiwa kuwa alikua akipanga njama za kuipindua serikali iliyopo madarakani.

Maafisa kadhaa kutoka chama tawala cha ANC wanapinga kuondolewa kwa waziri huyo Gordhan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *