Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu amefunguka kuwa kufanya Onesho zuri sio kitu cha Bahati bali ni kujituma na kufanya kazi kwa Bidii kwa ajili ya kupata mafanikio.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ameshare Show yake alioifanya Wikiendi iliyopita katika Tuzo za Soundcity MVP kisha kuisindikiza na Ujumbe huo.

Pia Zuchu amewataka wasanii wenzake kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuupeleka mbali muziki wa Bongo Fleva na kufahamika kimataifa na sio kubase ndani tu.

Mwanamuziki huyo kwasasa ni miongoni mwa wasanii wa kike wanaofanya vizuri Afrika Mashariki na katika kutokana na kazi zake za muziki wa Bongo Fleva.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *