Zuchu akataa bifu na Nandy

0
335

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu amefunguka na kusema kuwa hana tatizo na msanii mwenzake Nandy ila kinachotokea katika mitandao ya kijamii ni watu tu kuwashindanisha katika kazi zao.

Zuchu amesema kuwa wao wako vizuri na hata wakikutana wanasalimia Vizuri hawana tatizo lolote kabisa anashangaa watu wanavyosema kuwa wana tofauti bali tofauti yao iliyokuwepo ni kwenye kazi tu lakini siyo chuku za kimaisha.

Vilevile Zuchu ameongelea maneno ya Watu wanaosema kuwa anatengenezwa ili Kumshusha Nandy na kusema maneno hayo yanaongelewa na Watu wasio na Mapenzi Mema kwake ili tu kumtengenezea maadui ambao yeye hawaitaji .

Amesema kuwa huwezi Kuzuia watu kukushindanisha , kwasababu watakushindanisha tu Lakini nachukia maneno ya Watu wanaosema natengenezwa kumshusha Nandy.

Zuchu ambaye yupo chini ya lebo ya WCB inasemekana anapaishwa ili kumshusha Nandy kwenye tasni ya Bongo Fleva licha ya msanii huyo kupinga vikali.

LEAVE A REPLY