Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amemtumia ujumbe golikipa wa Manchester City, Claudio Bravo kupitia Facebook kufuatia mechi ya Manchester derby siku ya jumamosi.

Zlatan ambaye ni mfungaji anayeongoza kwa magoili kwenye klabu yake ameweka video kwenye ukurasa wake wa Facebook siku ya jana ambao unaonesha kumtisha kipa huyo wa Manchester City kwenye mechi yao ijayo ya ligi kuu itakayochezwa katika uwanja wa Old Trafford.

Claudio Bravo: Kipa wa Manchester City
Claudio Bravo: Kipa wa Manchester City

Golikipa huyo ambaye ni nahodha wa Chile alijiunga na Manchester City kwa ada ya uamisho ya paundi milioni 17 akitokea klabu ya Barcelona ya Uhispania na anatarajiwa kuanza kuitumikia City dhidi ya Manchester United siku ya jumamosi.

Kupitia ukurasa wake wa Facebiook, Ibrahimovic alituma video pamoja na maneno yafuatayo:  “Welcome to Manchester! Here’s some training gear, you’re gonna need it. See you Saturday.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *