Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema Tanzania inapaswa kuhakikisha sheria na sera za madini zinalazimisha rasilimali madini kuwa mali ya Watanzania ndipo nchi itanufaika.

Zitto amesema ni wakati muafaka kwa Taifa kujitoa katika mfumo wa kodi za Kimataifa akiuelezea kuwa umeonesha kunyonya nchi maskini zaidi na kunufaisha zile  tajiri.

Pia amesema kwa kuwa Rais John Magufuli ameamua kupigania vita hiyo ni jukumu la kila Mtanzania kupigana hadi kuhakikisha kuwa madini yanakuwa ni mali ya wananchi wa Kitanzania.

Zitto alisema kwa mujibu wa sheria iliyopo inaanisha kuwa baada ya mwekezaji kuingia mkataba na Serikali madini ni mali yake jambo ambalo halikubaliki.

Mbunge huyo amesema kwa mujibu ya sheria ya gesi na mafuta mwekezaji ni mkandarasi ambapo akipata bidhaa husika anarejesha gharama yane na katika faida nchi inagawana na mwekezaji kwa sawa au nchi kupata zaidi.

Pia asema jambo la pili ni mfumo wa kodi wa kidunia umeweka mazingira ambayo kampuni za Kimataifa zinauwezo wa kuhamisha mapato yake kwenda kwenye visiwa ambavyo kodi zipo chini hali ambayo inachangia wasilipe kodi.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *