Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa askari aliyemtishia bunduki aliyekuwa naibu waziri wa Fedha na Uchumi, Adam Malima achukulie hatua kwa kitendo hiko.

Kauli hiyo ya Zitto Kabwe imekuja baada ya Askari Polisi kumtishia bunduki Malima maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam.

Kitendo hiko cha askari aliyekuwa doria kimewashangaza wengi na kupelekea Raia wa maeneo hayo kutawanyika kutokana na milio hiyo ya risasi.

Zitto kabwe ameonyesha masikitiko hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii Facebook akihoji kama polisi wanafundishwa kuwafanyia hivyo raia wasiokuwa na hatia kiasi cha kuibua hofu katika jamii.

Zitto Kabwe ameandika “Hii ni nini ?, askari wetu wanafundishwa kufanya hivi, Waziri Mwigulu huyu yupo wazi na ni wa kutoka kwako. Unahitaji uchunguzi”.

Askari hao walioambatana na kampuni ya Majembe Auction Mart waliokuwa wakitaka kujaribu kukamata gari iliyokuwa imeegeshwa pembeni ya barabara ya Masaki karibu na Hoteli ya Double Tree.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *