Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemtetea Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na kusema kuwa anaamini Mbunge huyo wa Hai hajawahi kujihusisha na dawa za kuleva kwa namna yoyote.

Zitto ambaye ameambatana na Mbowe katika mkutano wake na wanahabari leo mjini Dodoma, amesema kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kumtaja Mbowe katika sakata la dawa za kulevya ni sawa na kutangaza vita na chuki dhidi ya chama hicho.

Mbunge huyo wa Kigoma Mjini amesema kuwakuichafua CHADEMA ni sawa na kuuchafua upinzani hivyo na yeye hawezi kukaa kimya kuona upinzani ukishambuliwa, na ndiyo sababu ya kuongeza nguvu kwa kuungana naye.

Mbowe ni miongoni mwa watu 65 waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaaam, Paul Makonda wanaojihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya hapa nchini.

Source: Global Publishers

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *