Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amekamatwa na jeshi la polisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) uliopo jijini Dar es Salaam akitokea Kigoma.

Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Chama Cha ACT Wazalendo, Abdallah Khamis ambapo baada ya kukamatwa kwa mbunge huyo.

Khamis amesema kuwa kiongozi huyo wa chama chake amekamatwa hivyo wanasheria wa chama hicho wanafuatilia kujua sababu ya kiongozi wa chama chao kukamatwa na jeshi la polisi.

Hata hivyo, kulikuwepo na taarifa za Katibu wa Bunge Dkt. Thomas kashililah kutoa amri kwa jeshi la polisi kumkamata Mbunge huyo wa Kigoma Mjini na kutakiwa kumfikisha mjini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na kauli ambazo amewahi kuzitoa juu ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *