Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema suala la mauaji yanayoendelea katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji, linahitaji mshikamano na kuwa mauaji hayo hayapewi nafasi ya kuendelea.

Zitto ameandika hayo leo kwenye ukurasa wake wa  facebook na twitter na kutaka taifa lizungumze lugha moja ili kukabiliana na mauaji hayo.

Zitto ambaye kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo amesema kuwa “Tunahitaji kushikamana Kama nchi kwenye suala la MKIRU ( Mkuranga, Kibiti na Rufiji ).

Pia ameendelea kwa kusema kuwa “Mauaji yanayoendelea huko hayapaswi kupewa nafasi kuendelea. Taifa lizungumze lugha moja kukabiliana na hali Hii”.

Zitto Kabwe ameandika hayo baada ya usiku wa kuamkia leo kuuawa kwa mtendaji wa kijiji wilani Kibiti mkoani Pwani.

Ameendelea kusema kuwa “Ninarejea wito niliotoa siku zilizopita kuwa Ninataraji Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama itakwenda Eneo la MKIRU kuzungumza na wananchi wa kule ili kupata maarifa ya mbinu za kuishauri na kuisimamia Serikali kudhibiti mambo na kuimarisha usalama”.

Amesema kuwa Naisihi Serikali itazame jambo hili la MKIRU ( Mkuranga, Kibiti na Rufiji) Kwa mtazamo mpana na wenye weledi. Tambo za IGP na Amiri Jeshi Mkuu zinaonekana ni maneno matupu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *