Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kupokea ripoti ya uchungzi wa mchanga wa madini kwenye makontena yaliyopo kwenye bandari hapa nchini, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa Tanzania ni tajiri kuliko Afrika Kusini kulingana na ripoti hiyo.

Kupitia akaunti yake Facebook, Zitto Kabwe ameandika kuwa “Mwaka 2016, Afrika Kusini ilizalisha tani 140 za dhahabu na Ghana tani 90 hivyo kuongoza Afrika”.

Zitto ameonegeza kwa kusema kuwa “Kwa Taarifa ya Prof. Mruma, Tanzania huzalisha tani 112  za dhahabu kutoka kwenye makanikia yaliyokutwa kwenye makontena ya migodi 2 tu ya Buzwagi na Bulyanhulu”.

Pia ameongeza kwa kuandika “Ukiongeza uzalishaji wa migodi ya North Mara na Geita, Tanzania inakuwa mzalishaji mkuu wa dhahabu Afrika nzima”.

Jana Rais Magufuli alipokea ripoti hiyo na kubaini madudu yanayotendeka ndani ya wizara ya Nishati na Madini mpaka kupelekea kufuta kazi Waziri wa Wizra hiyo Sospeter Muhongo.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *