Nchi ya Zimbabwe inatarajia kujenga chuo kwa gharama ya dola bilioni moja, kwa hemisha ya rais wa nchi hiyo Robert Mugabe.

Jonathan Moyo, ambaye ni waziri wa elimu aliwaambia waandishi wa habari kuwa wanachukua hatua hiyo kwa heshima ya rais huyo wa umri wa miaka 93, kwa wajibu wake katika elimu na uongozi mzuri.

Haijulikani pesa hizo zitatoka wapi kwenye nchi ambayo ukosefu wa ajira na umaskini ni tatizo kubwa.

Mwaka uliopita zaidi ya watu watu milioni moja nchini Zimbabwe walikumbwa na ukosefu wa chakula kotokana na ukame. Nchi hiyo wakati mmoja ilitajwa kuwa ghala la Afrika.

Haki miliki ya picha Reuters Image caption Milongo mirefu kwenye benki mjini Harare

Licha ya hilo baraza la mawaziri limekubali kutumia dola milioni 800 kujenga chuo hicho kipya huko Mazowe, kilomita 35 nje ya mji wa Harare.

Pesa zingine dola milioni 200 zimetengwa kwa utafiti katika chuo hicho cha Robert Gabriel Mugabe, kitakachoangazia masuala ya sayansi na teknolojia.

Tangazo hilo limekosolewa na vyama vya upinzani ambavyo vina matumaini ya kufikisha mwisho uongizi wa bwana Mugabe, wa miaka 37 wakati wa uchaguzi wa mwaka ujao.

Tayari Zimbabwe ina in wakati mgumu kugharamia elimu pamoja na huduma za umma na miundo msingi kama barabara na hospitali.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *