Jumla ya timu kumi na sita zimefuzu kwa hatua ya kumi na sita bora ya michuano ya klabu bingwa ulaya, huku timu zilizomaliza katika nafasi ya tatu katika kila kundi zitaenda kushiriki michuano ya Europa ligi.

Droo ya kupanga raundi ya mtoano ya timu kumi na sita itapangwa siku ya jumatatu Decemba 12.

Timu zilizofuzu kutoa kundi A ni Arsenal wakiwa vinara wa kundi na pili nafasi ya pili wako Psg, Kundi B vimefuzu timu za Napoli na Benfica.

Kundi C wamefuzu vigogo Barcelona na Manchester City huku kundi D kukiwa na Atletico Madrid na Bayern Munich.Kutoka kundi E zimefuzu Monaco na Bayer Leverkusen, na kundi F wamefuzu Borussia Dortmund na Real Madrid.

Leicester na Porto wamefuzu kutoa kundi G huku Juventus na Sevilla wakiwa wamefuzu katika kundi la mwisho kundi H.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *