Takwimu kutoka Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa wasichana wanauwezekano mara mbili zaidi wa kukosa masomo katika maeneo ya mizozo.

Katika baadhi ya nchi kama Syria, hakukuwa na takwimu za kubainisha ili kuwekwa katika orodha.

Wasichana wengi wadogo hufanya kazi badala ya kwenda shuleni. Na wengi huolewa wakiwa wachanga, na kuzima fursa yoyote ya kupata masomo.

Hizi hapa sehemu 10 ambapo wasichana hupata changamoto za kusoma:

  1. Sudan kusini: Zaidi ya robo tatu ya wasichana hawakufika shule ya msingi.
  2. Jamhuri ya Afrika ya Kati: kuna mwalimu mmoja kwa wanafunzi 80
  3. Niger: Asilimia 17 pekee ya wanawake kati ya miaka 15 na 24 wanaweza kusoma na kuandika
  4. Afghanistan: Kuna pengo kubwa la jinsia huku uwezekano wa wavulana kuwa shuleni kuliko wasichana ukiwa juu
  5. Chad: Masuala ya kijamii na uchumi inawazuia wasichana na wanawake kupata masomo
  6. Mali: Asilimia 38 pekee ya wasichana huweza kuhitimu kutoka shule za msingi.
  7. Guinea: wakati wastani wanaotumia wanawake zaidi ya miaka 25 katika masomo ni chini ya mwaka mmoja
  8. Burkina Faso: Asilimia 1 pekee ya wasichana humaliza masomo ya sekondari
  9. Liberia: Takriban theluthi mbili ya wanafunzi waliotimia umri wa kuenda shule za msingi hawaendi shuleni
  10. Ethiopia: Wasichana wawili kati ya watano wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18

Ukosefu wa walimu wa kutosha ni tatizo ambalo lilishuhudiwa kwenye nchi maskini.

Mwaka jana, Umoja wa Mataifa ulisema kuwa walimu milioni 69 zaidi, wanastahili kuajiriwa duniani kufikia mwaka wa 2030 ikiwa ahadi za kimataifa kuhusu masomo zitahitajika kutimizwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *