Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane ameafikiana na mabingwa hao wa Ulaya na Uhispania kuhusu mkataba mpya wa miaka mitatu.

Kiungo huyo wa kati wa zamani wa Real, katika katika miezi 18 ambayo amekuwa kwenye usukani, ameshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili na taji la La Liga mara mbili.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa mwenye miaka 45 alikuwa kocha wa timu B ya Real kabla ya kuchukua nafasi ya Rafael Benitez Januari 2016.

Real Madrid inatarajia kucheza dhidi ya Barcelona leo kabla ya mechi ya marudiano itachezewa Bernabeu Jumatano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *