Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kulitetea Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya timu yake Real Madrid kuibuka mshindi kwa ushindi wa 4-1 dhidi ya ipiga Juventus.

Zidane ameiongoza timu hiyo kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo.

Hivyo, rekodi ya kocha aliyebeba kombe hilo mara mbili au kulitetea inakwenda kwa raia huyo wa Ufaransa ambaye amewahi kuzichezea kwa mafanikio Juventus na baadaye Madrid.

Pia Zidane anaendelea kutunza rekodi yake aliyoiweka msimu uliopita akitwaa kombe hilo katika kofia mbili tofauti yaani akitwaa wakati akiwa kama mchezaji na baadae akitwaa akiwa kama kocha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *