Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameanza ziara yake katika wilaya Kinondoni ambapo asubuhi ya leo amezungumza watumishi wa wilaya hiyo pamoja na kutoa baadhi ya maagizo.

Makonda amewataka wakuu wa wilaya wote kuanzisha kitengo maalum cha kisheria kitakacho tumika kutoa elimu kuhusu migogoro ya ardhi na kuwashauri wananchi kabla ya kupeleka malalamiko yao mahakamani na kuwaweka wazi kama kuna dalili ya kushinda au vinginevyo na kuwapa suluhisho la kudumu.

Katika hatua nyingine RC Makonda amemtaka DC Hapi na Meya wa Kinondoni Bernard Sita kufuatilia suala la vibali vya ujenzi na kuhakikisha vinatoka kwa wakati ili kuharakisha maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DC Hapi amehaidi kuwashughukia watendaji wote watakao bainika kutowajibika kikamilifu ili kuchochea maendeleo.

Makonda anafanya ziara katika mkoa wa Dar es Saalaam ili kusikiliza kero zinazohusu wananchi katika mkoa huo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *