Zari asababisha Diamond kushangilia Uganda ‘Afcon’

0
617

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Diamond Platnumz amesema katika michuano ya Mataifa ya Afrika ‘Afcon’ inayoendelea nchini Gabon yeye anaishabikia timu ya taifa ya Uganda kutokana na Taifa Stars kukosa nafasi ya kushiriki.

Mkali huyo amesema kuwa sababu nyingine iliyosababisha kushangilia timu ya taifa ya Uganda ni kwasababu ni taifa analotoka mpenzi wake ambaye ni mzazi mwenzie wa watoto wawili, Zari the Boss Lady.

Pia Diamond amesema sababu nyingine iliyofanya aishabikie Uganda kwa sababu ni timu pekee inayoiwakilisha ukanda wa Afrika Mashariki kutokana na timu nyingine za ukanda huo kukosa nafasi.

Diamond alipata nafasi ya kutumbuza kwenye ufunguzi wa michauno hiyo siku ya Jumamosi Januari 14 mwaka huu akiwa na wanamuziki wenzake kama vile Mohombi na weningeo.

Timu ya taifa ya Uganda ipo kwenye kundi D ambapo leo itashuka dimbani kupambana na Ghana kwenye mehi yake ya kwanza kwenye michuano hiyo ya mataifa ya Afrika nchini Gabon.

LEAVE A REPLY