Zarina Hassan maarufu kwa jina la Zari thebosslady amepata dili la kutangaza magari aina ya Mercedez-Benz ya kampuni ya AMG Performance Centre iliyoko nchini Afrika ya Kusini.
Hayo yameonekana baada ya mwanadada huyo kuweka picha katika ukurasa wake wa Instagram gari nyeupe aina ya Mercedez-Benz huku akiwa amevalia suti yenye rangi ya zambarau.
Katika kurasa huo aliweka picha tofauti tofauti na kuandika maneno yafuatayo ‘amgperformancecentremenlyn is your centre for class & #stateTheArt cars. Thank you for the car’ na nyingine akiweka #closeDealsInHeels.
Baada ya ujumbe huo mashabiki wake wamempongeza kwa hatua hiyo hasa baada ya yote aliyoyapitia katika maisha yake ya mahusiano na msanii Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platnumz.