Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) imeangamiza zaidi ya tani 62 za vyakula vibovu na vilivyopitwa na wakati katika zoezi lililofanyika Kibele Mkoa Kusini Unguja.

Mkuu wa Idara ya Biashara na Uendeshaji wa ZFDB, Abdulaziz Shaib Mohd amesema bidhaa hizo mbovu zinatokana na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kujenga matumaini ya kuingiza faida kwa bidhaa wanazouza bila kuangalia usalama wa bidhaa hizo kwa afya za watumiaji.

Abdulaziz ambae pia ni Mkuu wa operesheni wa uangamizaji amesema bidhaa hizo zimegundulika kufuatia operesheni iliyofanywa na Bodi katika maghala na maduka mbali mbali ya Unguja.

Pia amesema ZFDB ambayo moja ya jukumu lake ni kusimamia ubora na usalama wa chakula, dawa na vipodozi kwa matumizi ya wananchi, itaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maghala yanayowekwa bidhaa na kwenye maduka ili kuhakikisha jukumu hilo linafanikiwa.

Vile vile amewataka wafanyabiashara kuwa wazalendo kwa wananchi wenzao na kujuwa kwamba biashara mbovu ama zilizopitwa na wakati ni sumu na zinaweza kudhofisha afya zao.Mkuu wa Idara ya Chakula bibi Aisha Suleiman amesema mchango mkubwa wa raia wema ndio uliofanikisha kugundulika bidhaa mbovu na zilizopitwa na wakati katika maduka na maghala mbali mbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *