Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo amesema kuwa Zanzibar wameanza kulipa deni awanalodaiwa na Tanesco.

Kauli hiyo ya waziri wa Nishati na Madini ameitoa Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano kati ya Rais wa Zanzibar, Mohamed Shein na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

Waziri huyo amewatoa hofu wananchi wa Zanzibar kuwa hawatakatiwa umeme, baada ya serikali ya mapinduzi Zanzibar kuanza kulipa deni hilo..

Prof. Muhongo amesema kuwa Zanzibar imeanza kulipa kiasi cha shilingi bilioni 10 na itaendelea kulipa deni hilo mpaka litakapomalizika.

Aidha Prof Muhongo ametoa wito kwa wadaiwa sugu wote wa TANESCO, kulipa madeni katika kipindi cha siku 5 zilizobaki kwa kuwa wasipolipa watakatiwa umeme.

Wiki chache zilizopita Tanesco ilitoa siku 14 kwa shirika la umeme la Zanziabr kulipa deni hilo wanaodaiwa zaidi ya miaka 20.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *