Chama tawala nchini Zimbabwe cha Zanu-PF kimeanza kukusanya michango kwaajili ya kusherehea kutimiza miaka 93 kwa rais wa nchi hiyo na mwenyekiti wa chama hicho, Robert Mugabe.

Mugabe anatarajia kutimiza miaka 93 baadae mwezi huu.

Chama hicho kimetangaza mpango wa kukusanya ng’ombe 150 kwaajili ya chakula.

Gazeti la serikali la Herald limemnukuu mbunge wa chama tawala cha ZANU-PF Never Khanye akisema kuwa utoaji huo ni hiari lakini wakulima wa mashamba makubwa kwenye eneo la Matabeleland Kusini ambapo sherehe hizo zitafanyika, ni lazima watoe ngome kuonyesha shukrani kwa kiongozi wa muda mrefu.

Tumeweka lengo la kupata ngombe 150 kwa sherehe hii. Tunawaomba wahisani watoe kwa mapenzi yao na wasije kesho kusema walilazimishwa’

Chama cha ZANU-PF kimesema kuwa kinatarajia watu 100,000 watahudhuria sherehe hizo zinazotarajia kufanyika kwenye eneo la Matobos nje kidogo ya mji mkubwa zaidi nchini humo wa Bulawayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *