Klabu ya Zanaco kutoka Zambia imewasili nchini kwa ajili ya mechi ya kombe la klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Yanga itakayofanyika siku ya Jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Zanaco imewasili leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNIA) wakiwa na viongozi wa timu hiyo.

zanaco-8

Timu hizo zitakutana kwenye mechi hiyo hatua ya mtoani baada ya kufanya vizuri kwenye mechi zao za awali zilizofanyika mwezi uliopita.

Kwa upande wa Yanga tayari wapo kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi hiyo itakayoamua nafasi ya kufuzu hatua inayofuta kwenye mashindano hayo ya klabu bingwa barani Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *