Matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais nchini Zambia yanaonyesha mgombea wa chama kikuu cha upinzani, Hakainde Hichilema anaongoza kwa ushindi wa kura chache.

Takwimu za Tume ya uchaguzi zinaonyesha Bw Hichilema yuko mpele ya Edgar Lungu rais wa sasa wa zambia kwa kura zaidi ya elfu sita.

Tume ya Uchaguzi ya Zambia ilipinga shutuma kutoka kwa Bw Hichilema kwamba ilikula njama na serikali ya kuchelewesha kutangaza matokeo ya uchaguzi.

Tume hiyo imesema ushiriki wa wapiga kura zaidi ya asilimia hamsina na saba unamaanisha kwamba shughuli ya kuhesabu kura itachukua muda kuliko ilivyo tarajiwa.

Edgar Lungu alichaguliwa mwaka jana kwa ushindi mdogo kufuatia kifo cha rais aliekuwepo mamlakani wakati huo, Michael Sata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *