Zahanati nchini India imejitolea kumsaidia mwanamme mrefu zaidi nchini ambaye aliambiwa kuwa kutokana na urefu wake, hawezi kufanyiwa upasuaji wa nyonga.

Daktari katika zahanati ya Speedy Recovery, amesema wanaweza kumsaidia Baraka Elias, ambaye madaktari wa hospitali ya Taifa Muhimbili wamesema hawezi kutosha katika kitanda cha hospitali hiyo.

Elias aliye na urefu wa futi 7.4 au mita 2.20 amesema anahitaji kufanyiwa upasuaji baada ya kuumia nyonga baada ya kuanguka.

Pia aliambiwa kuwa hasingeweza kutosha katika mashine ya X-ray kutokana na urefu wake kuwa tofauti na binadamu wengine.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *