Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Z Anto amesema alipata ofa ya kujiunga na WCB lakini alikataa kwa kuwa anataka kufanya kazi nje ya lebo hiyo.

Z Anto amesema kuwa mpaka sasa kuna label zaidi ya nne ambazo zinamuhitaji kufanya naye kazi lakini amekataa kufanya nao kazi kutokana na yeye kutokuwa tayari kufanya kazi na lebo hizo.

Mwanamuziki huyo ambaye aliwahi kutamba na nyimbo yake ‘Binti Kiziwi’ amesema alikuwa na maongezi na Babu Tale kuhusu kujiunga na WCB lakini amekataa ofa hiyo lakini yeye anatamani kufanya kazi nje ya lebo hiyo inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

Pia Z Anto amesema kuwa mafahari wawili hawawezi kukaa zizi moja na kufanya kazi pamoja kwa kuwa kila mtu ana hisia zake katika muziki kutokana na hayo hawawezi kufanya kazi pamoja na Diamond.

Z Anto ameongeza kwa kusema kuwa ukimya wake una mambo mengi mazuri kwasababu kuna lebo moja kubwa nchini ambayo yeye anatamani kufanya nayo kazi na mambo yanakwenda vizuri.

Mwanamuziki huyo alijizolea umaarufu kutokana na nyimbo zake kuwabamba mashabiki zake miaka ya nyuma ambapo alikuwa anamilikiwa na Babu Tale chini ya kundi la Tip Top Connection.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *