Rapa maarufu nchini Marekani, Young Thug amesema kuwa albamu yake mpya aliyoipa jina la ‘Jeffery’ itakuwa na nyimbo zenye maudhui kama alizokuwa akiimba mkali wa Pop, Michael Jackson.

Staa huyo amesema anachokiamini mwisho wa siku, kila mtu ataipenda albamu yake hiyo mpya kwakuwa hakuna wimbo wowote wenye maudhui kama mashabiki wake walivyomzoea kwenye nyimbo zake zilizopita.

Young Thug amesema ameamua kubadilika na kurudi kwenye asili yake ya uimbaji mbapo atakuwa anaimba Melody kama za Michal Jackson kwani ndiko alikoanzia kabla ya kuanza kurap.

MJ

Kwa upande mwingine Thug aliongeza kwa kusema kuwa hajawahi kuuza madawa ya kulevya kama anavyoandamwa kwenye mitandao ya kijamii na anataka kuachana na bifu anazoziita za kijinga dhidi yake na Lil Wayne pamoja na The Game.

Rapa huyo anatarajia kuachia mixtape ya albamu yake mpya kabla ya mwezi Septemba mwaka huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *