Mkali wa Hip-Hop nchini, Young Killer amefunguka na kusema kuwa yeye hana tofauti yoyote na msanii Baraka The Prince ambaye awali alishawahi kunukuliwa kuwa havutiwi na kazi za msanii huyo mwenzake kutoka Mwanza.

Young Killer amesema kuwa yeye hana tofauti yoyote na Baraka The Prince na kusema alisikia hizo tetesi lakini yeye anamkubali Baraka The Prince kutokana na kazi zake na uimbaji wake kwa ujumla.

barak-3

Staa huyo amesema kuwa yeye mwenyewe alisikia hizo tetesi mtaani lakini ukweli ni kwamba hana tofauti na Baraka The Prince na pia anakubali sana kazi zake pamoja na uimbaji wake mzuri.

Pia Young Killer amesema kwa sasa amerudia utaratibu wake wa zamani wa kutoa kazi kila baada ya miezi mitatu ili kuwa karibu na mashabiki wake kwa kuwapatia radha tofauti.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *