Staa wa Hip-Hop nchini, Young Killer amefunguka kwa kusema kati ya wasanii wenzake wenye umri kama wake Dogo Janja na Young Dee anamkubali na kumuelewa zaidi Dogo Janja.

Staa huyo amesema sababu za kumuelewa zaidi Dogo Janja ni kwasababu alimuhamasisha inawezekana kufanya muziki na kufanikiwa hata kama una umri mdogo.

Dogo Janja
Dogo Janja

Young Killer aliongeza kwa kusema kwamba kabla ajamsikia Dogo Janja akivuma kwenye muziki alidhani kwamba ili ufanye vizuri kwenye muziki ni lazima uwe mtu mzima,

Pia staa huyo amesema alivyomsikia Dogo Janja nikasema kumbe unaweza kutoka kimuziki hata kama una umri mdogo kwahiyo akaamua kuanza harakati za muziki mpaka sasa anajulikana nchini nzima kwa kipaji chake cha uimbaji.

Vile vile Young amesisitiza kwamba Young Dee ni muimbaji mzuri pia ila yeye anamkubali sana Dogo Janja.

Young Dee
Young Dee

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *