Wanamuziki wa hip hop wanaofanya vizuri kwasasa, Young killer na Dogo janja wamepigana vijembe huku kila mmoja akijitamba kuwa yeye ni mkubwa na bora kuliko mwenzake.
Kwa upande wake Dogo Janja amesema kuwa hajaona msanii wa kushindana nae kwa sababu yeye ndiye role model wa madogo wote walioimba muziki hata Young Killer yeye ndiye aliyemshawishi aingie kwenye muziki kwa hiyo
Dogo Janja ameendelea kusema kuwa dogo anayechana ni mmoja tu na ni yeye na Young Killer ndiyo niliyemuinspire kufanya muziki.
Kwa upande wa Young Killer amesema kuwa haoni kama dogo janja anaimba rap bali anaimba miziki yao ya kibiashara na yeye ngoma yake ya mwisho aliyofanya na Mr. Blue ndiyo aliyofanya rap kweli.
Pia Young Killer ameema yeye amewaachia mashabiki waseme wanaonaje kwa mtazamo wao kuhusu ubishani huo kati ya wawili hao.
Dogo Janja kwa sasa anatamba na nyimbo yake ‘Kidebe’ ambayo inaendelea kufanya vizuri huku Young Killer akitamba na nyimbo inayoitwa ‘Kumekucha’ aliyomshirikisha Mr Brue.