Staa wa miondoko ya Hip Hop nchini, Young Killer Msodoki amesema wimbo wake mpya ambao atauchia hivi karibuni utakuwa ni moja kati ya nyimbo zake bora kutokana na kubadilika katika uimbaji.

Young Killer amesema kuwa “Labda niwaambie kitu kimoja hii ni exclusive, ngoma yangu ambayo nitakuja kuitoa baada ya hii ‘Mtafutaji’ ndo ngoma yangu best kabisa,.

Pia amesema nyimbo hiyo itakuwa kali kuliko zote zilizopita, lakini hii inayokuja ni best kwa sababu ni ngoma kali kiukweli na anaamini watu watapenda.

Young Killer amesema hayo kutokana na uandishi pamoja na utunzia ndani ya nyimbo hiyo inayokuja huku akisisitiza mashabiki kuingojea nyimbo hiyo.

Mwanamuziki huyo amesema kabla ya kuachia wimbo huo ataachia kwanza video ya wimbo ‘Mtafutaji’ ambao aliuachia wiki chache zilizopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *