Mkali wa hip hop Bongo, Young Dee ametumia ukurasa wake wa Instahgram kufahamisha uma kuwa amevamiwa na kuporwa simu pamoja na pochi yake maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam.

Kupitia akaunti yake Instagram Young Dee amesema kuwa usiku wa juzi amevamiwa na mtu ambaye yeye anamuhisi kuwa ni Van Dame wa Sinza wakati akiwa studio kwa producer Mr T Touch akirekodi nyimbo.

Young Dee ameandika ‘Usiku Wa kuamkia juzi, tulivamiwa na jamaa anaesemekana ni Dame Wa sinza, nikiwa nimekesha studio maeneo ya sinza palestina kwa Mr T Touch”

Pia ameongeza kwa kuandika kuwa “Sasa juhudi za kumpata zimekua ngumu maana amekua na matukio ya hivo mara kwa mara juzi kaiba simu mbili moja ni yangu (iphone6s+) na Samsung na wallet yangu iliyokua na vitambulisho vyangu pamoja na Card ya bank, Sasa kwa yoyote ataepata taharifa itayoweza kunisaidia naomba anifate Dm tafadhari! ? Tag wana wote Wa sinza tusaidiane kwa hili!,

Young Dee amesema kuwa kwa yoyote atakaye okota kitambulisho chake atoe taarifa polisi kwani ni muhimu sana kwake.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *