Beki wa Yanga, Kevin Yondan ameanza mazoezi na timu yake baada ya kukosekana kwa wiki mbili kutokana na kuwa majeruhi.

Yondan aliumia wiki mbili zilizopita katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama iliyofanyika nchini Ghana ambapo Yanga ilifungwa 3-1.

Kelvin Yondani: Akiwafanya mazoezi.
Kelvin Yondani: Akifanya mazoezi.

Baada ya kukosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Yanga ikilazimishea sare ya 0-0, Yondan amerudi uwanjani baada ya kupona majeruhi.

Yondan amefanya mazoezi kikamilifu na timu yake katika Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam, kuelekea mchezo wa Jumamosi dhidi ya Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria Kombe la Shirikisho Afrika katika uwanja wa taifa.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *