Kada wa Chadema na mfanyabiashara, Yeriko Nyerere amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matano.

Baadhi ya mashtaka hayo ni kutoa taarifa za upotoshaji kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook mpaka kupelekea kukamatwa kwake.

Wakili wa Serikali, Elia Athanas alidai kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilabard Mashauri kuwa mtuhumiwa huyo alitenda makosa hayo kinyume na kifungu cha 16 cha Sheria ya Mtandao namaba 14 ya 2015.

Mtuhumiwa ameachiwa kwa dhamana baada ya kukidhi masharti ya dhamana hiyo kwa kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya milioni 10.

Kesi hiyo imehairshwa mpaka itakapotajwa tena Juni 5 mwaka huu katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kusutu jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *