Staa wa muziki nchini Nigeria, Yemi Alade amefanikiwa kupata mwaliko wa kuhudhuria katika sherehe ya utoaji waztuzo za ‘Annual Grammy Awards’ ambazo zitatolewa nchini Marekani Februari 12, mwaka huu.

Sherehe ya utoaji tuzo hizo zinatrajiwa kufanyika katika ukumbi wa Staples Center jijini Los Angeles nchini Marekani zikiwa ni tuzo za 59 toka zianze kutolewa.

Yemi Alade ambaye anafanya vizuri na nyimbo yake ‘Koffi Anan’ anapata nafasi hiyo kwa mara ya kwanza kuhudhuria tamasha hilo kubwa duniani.

Mwanamuziki huyo kupitia akaunti yake ya Instagram akusita kuweka wazi mwaliko huo na kuwashukuru wote ambao walimuunga mkono kwa mwaka 2016 na wanaondelea kumuunga mkoni hadi sasa.

Kupitia ukurasa wake huo wa Instagram Yemi Alade ameandika “Naamini nafasi hii nimeipata kutokana na kujituma kwangu mwaka 2016 pamoja na mashabiki wangu kuonyesha kunijali, ninawashukuru wote kwa kunijali na kupenda muziki wangu,” .

Tuzo za Grammy ni tuzo kubwa za muziki duniani ambazo hutolewa kila mwaka mnamo mwezi wa Februari kwa ajili ya kuwatunukia tuzo wanamuziki waliofanya vizuri katika suala zima la uimbaji.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *