Mwanamuziki nyota wa Nigeria, Yemi Alade amesema kwamba msanii anayetamani kufanya nae nyimbo katika ukanda wa Afrika Mashariki kwasasa ni Ali Kiba kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kuimba.

Yemi Alade aliyasema hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha ‘The Sporah show’ baada ya kuulizwa msanii gani anayetamani kufanya nae nyimbo ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Alikiba
Alikiba

Kwa upande wa wasanii wa kimataifa, Yemi Alade amesema anatamani kufanya nyimbo na mwanamziki, Nick Minaj kwa kuwa ndiye anayemkubali sana kutokana na uwezo wake wa kuimba mwingine anayetaka kufanya naye ni Beyonce.

Yemi Alade ni mwanamuziki aliyejizolea sifa kwa mashabiki wake wa Afrika kutokana na nyimbo zake kuwa kali na kupelekea kuchukua tuzo za MTV MAMA.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *