Mwanamuziki wa Nigeria, Yemi Alade amevijia juu vyombo vya habari nchini humo baada ya kuvishtumu kwamba vinagombanisha wasanii wakubwa wa kike.

Yemi Alade ameyasema hayo baada ya vyombo vya habari kumgombanisha na msanii mwenzake wa kike nchini humo Tiwa Savage kutokana na upinzani uliopo katika ya wawili hao katika anga ya muziki wa Ningeria na Afrika kwa ujumla.

Yemi Alade aliyazungumza hayo wakati akifanyiwa mahojiano na kusisitiza kuwa hana tofauti na wala ukorofi na wasanii wenzake wa kike kama Chidma, Seyi Shay na Tiwa Savage ambao ndiyo wapinzani wake kwasasa.

Mshindi huyo wa tuzo ya mwanamuziki bora wa kike Afrika wa MTV amesema kuwa yeye alianza kuimba hata kabla Tiwa Savage ajaenda Nigeria hivyo hawezi kuwa na tofauti na mwanamuziki huyo.

Kwa upande mwingine Yemi Alade amesema kuwa yeye na Tiwa Savage si marafiki lakini hawana beef kabisa kwasababu kila mwanamuziki anamaisha yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *