Klabu ya soka ya Yanga imeweka wazi viingilio vya mchezo wao wa mtoano dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia.

Katika viingilio ambavyo Yanga imevitaja leo, shilingi 3,000 ndio kiingilio cha chini zaidi ambacho kitatumiwa na mashabiki wanaotaka kutazama mechi hiyo wakiwa kwenye jukwaa la mzunguko.

Kwa wale watakaoketi kwenye jukwaa la VIP B na C kwenye uwanja wa taifa watalazimika kupata tiketi kwa shilingi 15,000 huku wale watakaoketi jukwaa kuu yaani VIP A watapata tiketi kwa shilingi 30,000.

Mchezo huo wa kwanza wa kuwania kufuzu hatu ya makundi ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa ngazi ya vilabu Barani Afrika utapigwa Jumamosi kuanzia saa 10:00 jioni.

Yanga kwasasa imeweka kambi yake mkoani Morogoro na inatarajiwa kutua jijini Dar es salaam kesho Alhamisi, tayari kwa mchezo huo ambao ni muhimu kwa Yanga ambayo msimu wa 2015/16 ilifuzu hatua ya makundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *