Klabu ya Yanga imepokewa kishujaa katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere (JNIA) wakitokea Mwanza ambako wamecheza mechi ya mwisho dhidi ya Mbao FC.
Katika mechi hiyo iliyofanyika jana katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Yanga walipoteza mechi hiyo kwa 1-0 lakini haikuzuia Yanga kutwaa ubingwa.
Baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam leo Yanga walipokewa na mashabiki zake waliojitokeza katika uwanja huo wa ndege jijini Dar es Salaam.
Msafara huo umeelekea hadi makao makuu ya labu hiyo yaliopo maeneo ya mitaa ya Twiga na Jangwani Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Yanga wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kufungana point na klabu ya Simba tofauti ikiwa na magoli.