Klabu ya Yanga imemtimua kazi mkurugenzi wake ambaye alikuwa kocha wa timu hiyo, Hans van Pluijm kutokana na kukumbwa na ukata wa kifedha.

Katibu mkuu wa timu hiyo Boniface Mkwasa amesema sababu za kukatisha mkataba na Pluijm kutokana na tatizo la kifedha linaloikumba klabu hiyo baada ya Mwenyekiti wake Yusuph Manji kuwa katika kipindi kigumu kwa sasa kwasasababu ya kukabiliwa na kesi.

Mkwasa amesema kuwa “Uongozi wa juu umeamua kusitisha kibarua cha Mkurugenzi wetu wa ufundi, kutokana na ukata wa fedha ambao unatukabili hivi sasa.

Ameongeza kwa kusema kuwa ‘Ni kitu ambacho kinaumiza kutokana na mchango wa Pluijm kwenye kikosi chetu lakini hatuna namna.

Pluijm aliifundisha Yanga kwa vipindi viwili tofauti huku akiisaidi timu hiyo kushinda mataji kadhaa ikiwemo mawili ya ligi kuu, Ngao za hisani (2), Kombe la FA mara moja na kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Africa CAF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *