Yanga leo imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji raia wa Zambia, Justice Zulu baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo.

Zulu alieyetua nchini usiku wa kuamkia Jumannne, amejiunga na Kocha George Lwandamina ambaye naye ni raia wa Zambia aliyewahi kufanya kazi pamoja na kiungo huyo.

Kiungo huyo tayari amewaahidi mashabiki na wapenzi wa Yanga makubwa ila wampe muda na watafurahi wenyewe.

Klabu hiyo inajikamilisha kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara pamoja na michuano ya kimataifa itkayoanza mwakani.

Yanga kwasasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara ikiwa nyuma ya Simba kwa tofauti ya alama mbili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *