Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportPesa ya nchini Kenya imetia saini mkataba wa kuidhamini Klabu ya Yanga kwa miaka mitano.

Katika Mkataba uliosainiwa leo, mwaka wa kwanza Yanga watanufaika kwa kupata Tsh. milioni 950 ambapo ndani ya miaka mitano watapata zaidi ya Tsh. bilioni 5.

Katika mkataba huo, Yanga watavaa jezi zenye nembo ya SportPesa kutokana na mkataba huo waliosaini leo.

Mkataba huo wa Yanga unakuja kufuatia makubaliano ya pande mbili kati ya kampuni hiyo na klabu ya Yanga.

Yanga inafuata nyayo za wapinzani wao klabu ya Simba ambayo iliingia mkataba na kampuni hiyo wiki iliyopita.

Kampuni ya SportPesa ni kampuni ya kamali nchini Kenya ambapo pia wanaidhamini klabu ya ligi kuu nchini Uingereza ya Hull City na sasa inatarajia kuingia mkataba na Everton.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *