Klabu ya Yanga SC imeondoka leo kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui.

Kikosi cha Yanga kilichokwenda Shinyanga ni Makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Benno Kakolanya na Deo Munishi ‘Dida’, mabeki; Hassan Kessy, Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Vincent Bossou, Andrew Vincent ‘Dante’ na Pato Ngonyani.

Viungo ni Said Juma ‘Makapu’, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Geoffrey Mwashiuya, Simon Msuva, Obrey Chirwa, Yussuf Mhilu, Juma Mahadhi na washambuliaji Matheo Anthony, Malimi Busungu, Amissi Tambwe na Donald Ngoma.

Mbali na mchezo wa Yanga dhidi ya Mwadui mechi zingine zitakuwa zikichezwa katika viwanja tofuti mwisho wa wiki hii ambazo ni Azam FC watamenyana na Simba SC uwanja wa Uhuru, Mbeya City na Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Mtibwa Sugar na Kagera Sugar Uwanja wa Manungu Morogoro, Ruvu Shooting na Mbao FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Maji Maji na Ndanda FC Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Jumapili kutakuwa na michezo miwili Stand United wakiikaribisha JKT Ruvu Stars Uwanja wa Kambarage, Shinyanga na African Lyon wakimenyana na Toto Africans Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *