Yanga SC na Azam FC leo zinashuka dimbani kucheza mechi ya ngao ya jamii kuashiria kuanza kwa ligi kuu Tanzania Bara ambapo mechi hiyo itafayika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Yanga itawakosa wachezaji wake wa tano muhimu ambao wanasumbuliwa na majeruhi kama vile kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ anayesumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu, mabeki Juma Abdul, Andrew Vincent ‘Dante’ wanaosumbuliwa na maumivu ya miguu, Kevin Yondani anayeumwa jicho na kiungo Obrey Chirwa anayeumwa goti.

Kwa upande wa Azam Fc wao wapo vizuri kukabiliana na Yanga SC baada ya beki wake kisiki Shomari Kapombe kupona majeruhi na leo anatarajia kuanza kwenye kikosi hicho cha mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati.

Timu hizo kwa mara ya mwisho zilikutana katika fainali ya kombe la TFF ambapo Yanga SC waliibuka na ushindi wa jumla ya mgoli 3-1 kwenye mechi hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Taifa.

Pia timu hizo zilikutana kwenye mechi ya ngao ya jamii msimu uliopita na Yanga kuibuka na ushindi wa jumla ya penati 8-7 baada ya kutoka sare ya 0-0 ndani dakika 120 za mchezo huo.

Kwa upande mwingine Ofisa Habaro wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Alfred Lucas amesema mapato ya mechi hiyo watanunua madawati kama mchango wa Shirikikso hilo katika juhudi za kuunga mkono uchangiaji wa madawati katika shule hapa nchini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *