Yanga ‘uso kwa uso’ na Mtbwa Sugar leo

0
324

Yanga leo itashuka dimbani dhidi ya Mtimbwa Sugar kweye mechi ya Ligi kuu Tanzania Bara katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa kikosi chake kiliweza kufika salama Morogoro na jana walifanya mazoezi katika uwanja huo ili wachezaji waweze kuuzoea uwanja pamoja na kuizoea hali ya hewa ya Morogoro.

Mwambusi amesema kuwa “Tunashukuru Mungu kikosi kipo salama na tulifanya mazoezi jana jioni hapa Morogoro, lakini jua la hapa tofauti kidogo na Dar es Salaam hivyo wachezaji wamefanya mazoezi vyema ili kuhakikisha wanauelewa uwanja kwanza.

Ameongeza kwa kusema kuwa harafu vile vile hali ya hewa ya Morogoro, tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe uzima ili tuweze kupambana na Mtibwa leo na kutafuta pointi tatu muhimu kwetu”.

Mbali na hilo viongozi wa Yanga wamesema kuwa dhamira yao ni kutetea ubingwa na kuhakikisha kombe la Ligi Kuu Bara linabaki Yanga tena.

LEAVE A REPLY