Klabu ya Yanga leo inashuka dimbani kumenyana na timu ya Jamhuri ya Pemba kwenye mechi ya kombe la Mapinduzi itakayofanyika katika uwanja wa Jamhuri visiwani Zanzibar.

 Azam FC watacheza na Zimamoto kuanzia Saa 10:00 jioni katika uwanja huo huo wa Aman visiwani Zanzibar

Mechi hizo zinafuatia mechi za ufunguzi za Kundi A zilizoanza Ijumaa Taifa Jang’ombe ikiilaza 1-0 Jang’ombe Boys.

katika mechi za jana wenyeji KVZ walianza vibaya baada ya kufungwa 2-0 na mabingwa watetezi, URA wakati vinara wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Simba wakiichapa 2-1 Taifa Jang’ombe.

Kwa sasa Simba inashika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi B ikiwa nyuma ya URA lakini timu zote tatu yaani Simba, Taifa Jang’ombe na URA zina point 3 kila moja.

Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu Mzambia, George Lwandamina imepania kufanya vizuri kwenye michuano ya mwaka huu baada ya kutokuwa na matokeo mazuri kwa miaka minne iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *