Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma anatarajia kukaa nje ya uwanja kwa wiki moja baada ya kuumia katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

Ngoma aliondoka uwanjani akiwa anachechemea dakika ya 77 na nafasi yake kuchukuliwa na Juma Mahadhi ambapo Yanga ililazimishwa sare ya kutofungana na Mtibwa katika mchezo wa ligi kuu ya VPL uliopigwa siku ya Jumamosi.

Baada ya mchezo huo Ngoma alipimwa na kugundulika kuwa misuri ya ndani ya paja ilivutika siku hiyo na kumsababishia maumivu kwa mujibu wa Daktari wa Yanga Edward Bavu.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa maiaka 28 alijiunga na klabu ya Yanga mwaka 2015 na amekuwa akicheza kwa kiwango cha juu.

Mpaka sasa Yanga wanashika nafasi ya 6 katika ligi kuu ya soka ya Tanzania bara wakiwa wamecheza michezo mitano na kukusanya jumla ya pointi 9 wakati watani wao wa jadi Simaba wakiongoza msimamo wa ligi kuu kwa pointi 11.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *