Klabu ya Yanga leo watacheza dhidi ya Stand United kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania Bara katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

 

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema, anaamini kikosi kipo imara kwa ajili ya mchezo huo ambao kwa upande wao ni mgumu na unawalazimu kushinda ili kupata pointi tatu huku akiwataka wanachama kuwa na umoja ili kuendelea kuipa timu sapoti katika michuano ya ligi pamoja na klabu bingwa Afrika ambayo inaanza hivi karibuni.

 

Mkwasa amesema, ligi inazidi kuwa ngumu katika mzunguko wa lala salama kutokana na kila timu kuhitaji kubaki katika nafasi nzuri huku akiongeza kuwa katika kila mchezo hususani kwa mchezo wa leo watacheza kwa kuhakikisha wanaibuka na ushindi ili kuweza kuhakikisha wanakuwa juu.

 

Yanga inaongoza ligi hiyo tofauti ya alama mbili dhidi ya wapinzani wao wa jadi timu ya Simba ya jijini Dar es Salaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *