Yanga leo itashuka dimbani kuwakaribisha Ruvu Shooting kwenye mechi ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Yanga chini ya kocha wake Hans Van Pluijm inashuka dimbani baada ya wiki iliyopita kupata ushindi mwembamba dhidi ya Tanzania Prisons na kufikisha alama 30.

Vinara wa ligi hiyo Simba walipoteza mchezo jana huko mkoani Mbeya dhidi ya Tanzania Prison kwa mabao 2-1 na kuwa mchezo wao wa pili kupoteza.

Azam FC wao wakicheza ugenini Mkoani Shinyanga walishinda kwa ushindi mnene wa mabao 4-1 dhidi ya Mwadui.

Msimamo wa ligi ulivyo Simba wanaongoza ligi wakiwa na alama 35, wakiwa wamecheza michezo 15, Yanga wako nafasi ya pili kwa alama 30 wakiwa wamecheza michezo 14.

Azam ana alama 25 nafasi ya tatu huku wakiwa wamecheza michezo 15. Kagera Sugar wana alama 24 kwa michezoi 15 wako nafasi ya nne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *