Uongozi wa Yanga leo umetangaza viingilio vya mchezo wao dhidi ya Ngaya kutoka Comoro kwenye mechi ya marudiano ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika uwanja wa taifa siku ya jumamosi.

Afisa Masoko wa klabu hiyo Omar Kaaya amesema kuwa kiingilio cha chini kitakuwa shilingi elfu tatu kwa majukwaa ya mzunguko na viti vya machungwa huku VIP A itakuwa sh. 20,000, VIP B sh. 10,000 na VIP C itakuwa sh. 10,000.

Kaaya amewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza uwanjani kwa winigi ili kuisapoti timu yao kwenye mechi hiyo

Kwa upande wake kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa katika mechi hiyo wataingia kwa ajili ya kupambana na si kuridhiaka na matokeo yaliyopita bali kuhakikisha wanapata ushindi mwingine.

Klabu ya Ngaya imewasili nchini kwa ajili ya mechi hiyo ya marudiano ya klabu bingwa Afrika baada ya kukubali kichapo cha goli 5-1 kwenye mechi ya kwanza iliyofanyika nchini Comoro wiki iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *